Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho ataka Simba iheshimiwe

Bocco Robertinhooo Robertinho ataka Simba iheshimiwe

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema, kesho wanakutana na mpinzani mgumu [Al Ahly] wanamheshimu lakini kwa sasa kila mpinzani anapaswa kuiheshimu Simba pia.

“Tuna timu nzuri, tunaheshimu kila mpinzani aliyepo mbele yetu, kesho ni fursa nzuri kwa wachezaji wangu kucheza mechi kubwa. Tunaiheshimu Al Ahly kwa sababu ina wachezaji wengi wenye uzoefu mkubwa lakini pia kila timu inapaswa kuiheshimu Simba.”

“Kama nilivyosema awali Al Ahly ni timu kubwa, ina mafanikio zaidi Afrika lakini kesho tunahitaji kuonesha uwezo wetu. Kwangu mchezo wa mpira wa miguu sio kama kupigana bali ni sanaa, kesho itakuwa ni mechi nzuri.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live