Kocha Mkuu wa Simba Mbrazil, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ametamka kuwa hatima ya wao kufuzu kucheza hatua Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ipo mikononi mwa wachezaji wao.
Hiyo imekuja ni baada ya timu hiyo, kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa wakiwa na pointi 9 katika Kundi C.
Simba amepangwa kukutana na Wydad Casablanca katika robo fainali mara baada ya droo kuchezeshwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) jana usiku.
Akizungumza nasi, Robertinho alisema kuwa, kikosi chao kina nafasi ya kufika mbali katika michuano ya kimataifa katika, lakini kama wachezaji wake wataendelea kufuata maelekezo yake anayowapa mazoezini.
Robertinho alisema kuwa amefuraishwa na namba ya wachezaji wake walivyocheza vizuri katika hatua ya makundi ya michuano hayo makubwa na kufanikiwa kufuzu robo kwa kila mmoja kutimiza majukumu yake ya uwanjani.
Aliongeza kuwa anaamini kama wachezaji hao wakiendelea kucheza kimbinu kwa zile ambazo anawapatia, basi ana matumaini makubwa ya timu yao kufika nusu.
“Wachezaji ndio watakaotuvusha kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sio mtu mwingine kwani wao ndio wanaocheza uwanjani.
“Tutafuzu kucheza fainali kama wachezaji wangu watacheza kwa kufuata maelekezo yangu ya kimbinu ambayo nimekuwa nikiwapa mazoezini.
“Katika hatua hii ya makundi, vijana wangu wamecheza wachezaji vizuri, nimefuraishwa na hamasa ya kila mchezaji aliyekuwepo uwanjani, hivyo ninaamini kama wakiendelea kucheza hivi, basi tunacheza fainali,” alisema Robertinho.