Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho ataja sababu kumuingiza Nyoni mechi ya Vipers

Robertinho Aiwahi Singida Big Stars Robertinho ataja sababu kumuingiza Nyoni mechi ya Vipers

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' amesema katika mchezo wa juzi dhidi ya Vipers kipindi cha pili, alilazimika kumuingiza kiraka Erasto Nyoni ili kutuliza mashambulizi baada ya wapinzani wao hao kurudi kwa kasi.

Robertinho amesema Erasto ni bora kwenye kuituliza timu inaposhambuliwa pia anapiga pasi ambazo hazipotei na hilo lilimfanya kumuingiza na ameisaidia timu.

"Tuliingia kwa lengo ;a kutafuta alama tatu na tunashukuru tumefanikiwa kuzipata. Tulimuingiza Nyoni kipindi cha pili ili kuituliza timu kutokana na kasi ambayo walirudi nayo Vipers," alisema Robertinho.

Akizungumzia mchezo wa marudiano nyumbani, Robertinho amesema anahitaji kupata ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuvuka hatua ya makundi.

"Ni jambo zuri kushinda nyumbani, jambo zuri itakuwa tunacheza mbele ya mashabiki wetu," alisema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live