Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho astukia jambo Simba, aja na mkakati huu!

Simba SC Uganda 1140x640 Kikosi cha Simba kina kazi ya kuhakikisha wanashinda dhid ya Vipers Machi 7

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Simba kuichapa Vipers bao 1-0 ugenini Uganda wikiendi iliyopita na kupewa mapumziko ya siku moja, Mnyama anarejea mazoezini Jumatatu jioni huku Mbrazili Roberto Oliveira 'Robertinho' akiingia na mpango kazi mpya wa mabao wa kuongeza idadi ya mabao kwani ameshtukia kitu.

Hiyo ni baada ya Simba kuonekana kupunguza kasi ya kupachika mabao, ikiwa imefunga mawili tu katika mechi nne zilizopita, tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika na moja dhidi ya Azam iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 ambalo hata hivyo ni la kujifunga kwa beki Abdallah Sebo hivyo kiuhalisia wachezaji wa Simba katika mechi nne za mwisho wamefunga bao moja tu.

Simba imekuwa ikitengeneza baadhi ya nafasi lakini washambuliaji wake wakiongozwa na nahodha John Bocco, Jean Baleke, Habib Kyombo na Moses Phiri kushindwa kuzitumia katika nyakati tofauti jambo lililogunduliwa na benchi la ufundi la chama hilo na kueleza mabadiliko makubwa yanaenda kufanyika.

Kocha Robertinho ameliambia Mwanaspoti, vipaumbele vyake ni timu icheze vizuri, kwa kasi na ipate ushindi lakini pia anafurahi ikishinda mabao mengi huku akigusia michuano ya CAF ambayo anaamini mabao yana faida zaidi.

"Pamoja na ushindi ugenini lakini bado tuna tatizo katika eneo la mwisho. Baadhi ya nafasi tunazotengeneza zinapotea hilo linamuumiza kila mtu kati yetu na tunaenda kulifanyia kazi licha ya kwamba tumeshajua wapi tunaanzia," alisema Robertinho na kuongeza;

"Katika mashindano yote tuliyopo tunahitaji mabao, hususani haya ya CAF ndio tunahitaji kufunga zaidi kwani inaweza kufika sehemu mkalingana alama na mwenzako na kitakachoamua kikawa mabao.

"Hivyo lazima tufanye kazi juu ya hilo, wachezaji wote kwa pamoja tutawaeleza mahitaji yetu na faida za kupata mabao na mwisho tutaenda kwenye uwanja wa mazoezi kutekeleza hilo kwa vitendo,"alisisitiza.

Simba inacheza na African Sports Alhamisi hii kwenye mechi ya FA na baada ya hapo itarudiana na Vipers Machi 8 kwa Mkapa kisha itaivaa Mtibwa Sugar kwenye Ligi Kuu Machi 11, 2022.

Robertinho hadi sasa ameiongoza Simba kwenye mechi sita, tatu za Ligi Kuu na tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika na kufunga jumla ya mabao sita ambayo ni wastani wa bao moja kwa kila mechi.

Mabao hayo ni 3-2 dhidi ya Mbeya City, 1-0 mbele ya Dodoma, na sare ya 1-1 na Azam huku kimataifa likiwa lile moja na la ushindi mbele ya Vipers.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live