Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho ashtukia jambo Power Dynamos, apangua kikosi tena!

Simba Power Ms.jpeg Robertinho ashtukia jambo Power Dynamos, apangua kikosi tena!

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wakijiandaa kuvaana na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa leo Alhamisi, Kocha Mkuu wa Simba Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameweka wazi kwamba anatarajia kufanya mabadiliko kidogo ya kikosi chake ili kupata uwiano mzuri kuelekea mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos.

Simba leo Alhamisi watashuka Uwanja wa Uhuru, kuvaana na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kabla ya kuwakaribisha Power Dynamos katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kusaka tiketi ya hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Ikumbukwe kwamba, mchezo wa kwanza ambao Simba walicheza ugenini nchini Zambia, walifanikiwa kupata matokeo ya sare mabao 2-2.

Akizungumza nasi, Robertinho alisema: “Licha ya matokeo ya sare ambayo tumeyapata Zambia ni kweli hatujaridhishwa na kiwango tulichoonesha hususani kutumia nafasi ambazo tulitengeneza.

“Sasa tunakuja kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo tunapaswa kurekebisha makosa ya mchezo wetu uliopita na kutumia kila nafasi ambayo tutatengeneza kupata mabao, sambamba na hilo tunatarajia kuwa na mabadiliko kidogo ya kikosi kutokana na ratiba za michezo yetu hii miwili.

“Tumekuwa na ratiba ya michezo kufuatana, hivyo ni lazima tutawapumzisha baadhi ya wachezaji na kutumia wengine kulinganisha na mchezo dhidi ya Power Dynamos ili kuwa na uwiano mzuri wa kikosi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live