Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho apiga "Stop" usajili wa Golikipa Simba

Robertinho X Bocco Kocha wa Simba, Robertinho

Fri, 19 May 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameshafunga msimu licha ya Ligi Kuu Tanzania Bara kusaliwa na mizunguuko miwili, na tayari ameshakabidhi ripoti kwa mabosi wa timu hiyo akielekeza usajili anaoutaka huku akiwazuia kabisa kumsajilia Mlinda Lango kwa madai analo chaguo lake.

Robertinho ameuambia uongozi wa Simba SC katika eneo la Mlinda Lango wasiwe na wasiwasi naye, kwani atawaletea nyanda ambaye ana kiwango bora cha kuwania au hata kumpora namba Mlinda Lango chaguo la Kwanza wa sasa, Aishi Manula na mazungumzo ya kumsajili mmoja kati ya Walinda Lango wawili ambao majina yao yapo mezani usitishwe.

Kuna majina mawili yanayotajwa yote kutoka Vipers akiwamo Mrundi Fabien Mutombo na Alfred Mudekereza, na inaelezwa jina moja ndilo ambalo Robertinho anà faili lake kwa sasa, huku orodha hiyo amependekeza kwa kila eneo ni kuletwa viungo wakabaji wapya wawili, viungo washambuliaji wawili, beki wa kushoto, beki wa kati wawili, winga asilia wawili na mshambuliaji mmoja.

Taarifa kutoka ndani ya Simba SC mezani kwa viongozi wa klabu hiyo kuna jina la Mlinda Lango kutoka taifa kubwa kisoka barani Afrika ambaye ana uzoefu na michuano ya kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu ya taifa na anaonekana yuko tayari kuitumikia miamba hiyo ya Msimbazi lakini kutokana na zuio la Robertinho, mabosi klabu hiyo wameamua kutoendelea na ushawishi wa kumleta nchini.

“Ni Mlinda Lango mkubwa na angekuwa msaada mkubwa kwa Simba SC kwani angekuja kushindania namba moja na ikiwezekana hata kumuweka benchi Aishi Manula lakini uongozi tayari umeshaambiwa waachane naye.” Ameeleza mtoa taarifa hizi

Wakati huo huo Wachezaji ambao wnatajwa huenda wakaachwa Simba SC mwishoni mwa msimu huu ni Gadiel Michael, Jonas Mkude, Ismail Sawadogo, Agustine Okrah, Peter Banda, Jimmyson Mwanuke, huku Moses Phiri na Joash Onyango wakitajwa kuomba kutaka kuondoka kikiosini wenyewe.

Chanzo: Dar24
Related Articles: