Jana kocha wa Yanga alilazimika kumpanga Gift Mauya badala Khalid Aucho katika kiungo cha chini. Doctor Aucho ndiye mchezaji muhimu zaidi Yanga, tayari ana kadi mbili za njano na kama jana angeona kadi nyingine basi angewakosa Simba.
Pacha wake katika kiungo, Mudathir Yahya na yeye ilibidi aende benchi mapema ili kumuweka fiti kwa ajili ya mechi ijayo. Kama ilivyo kwa Aucho, unamuhitaji Mudathir bora wakati wote ili kiungo cha Yanga kisogee..
Baada ya kuongoza mabao mawili Yanga waliamua kupunguza kasi ya mchezo. Wakajihami kwa kumiliki mpira, wakapunguza kukimbia ili kutunza nguvu kwa ajili ya mechi ijayo. Kumbuka bado walikuwa na ratiba ngumu sana hadi kufika jana.
Kama ilivyo kwa Yanga, Simba wamecheza mechi ngumu mfululizo na wametumia nguvu kubwa. Mbaya zaidi hawajapata nafasi ya kubadilisha/kuwapumzisha wachezaji wao wengi. Ni Henock Inonga pekee ambaye hajacheza 'panga pangua' katika kikosi cha Simba na ni kwasababu ya majeraha.
Mechi muhimu dhidi ya Ihefu nasubiri kuuona mkakati wa Robertinho. Kusaka pointi tatu na hapohapo kujiandaa na mchezo wa Yanga. Maamuzi gani atachukua Robertinho? Ukivaa viatu vyake unaona maamuzi yapi ni sahihii zaidi kwake??