Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho ameongoza kwa kufanyiwa mahojiano jana-Ahmed

Roberto Oliveira, Robertinho Kwa Robertinho ameongoza kwa kufanyiwa mahojiano jana-Ahmed

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka Morocco zimeeleza kuwa, Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' alifanyiwa mahojiano zaidi mara baada ya mechi ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa kukamilika.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulipigwa usiku wa kuamkia leo, Aprili 29, 2023 katika dimba la Mohamed V nchini Morocco.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema, ilikuwa ni mshangao wa aina yake baada ya Simba kuikazia Wydad hadi kufikia hatua ya kupiga matuta baada ya mchezo kuisha kwa Wydad kufunga 1-0.

Mchezo wa awali uliopigwa Benjamini Mkapa Stadium, Simba nao waliondoka na ushindi wa 1-0 hivyo kwenda kwenye mikwaju ya pelnati na Simba kuondoshwa baada ya kukosa mikwaju miwili.

"Waandishi walitamani kujua amewezaje ndani ya muda mfupi kutengeneza Simba yenye ubora tuliokuwa nao. Wandishi wa vyombo vikubwa hapa Morocco walimfuata mara tu baada ya mechi kuisha," alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live