Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho amchimba mkwara Okrah

Okrah Kituu Augustine Okrah

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera 'Robertinho' amempiga mkwara mzito nyota wa timu hiyo, Augustine Okrah kwa kumtaka ili aingia kwenye kikosi chake ni lazima ahakikishe anakuwa fiti asilimia 100 na siyo vinginevyo.

Robertinho alisema ili mchezaji apate nafasi ya kucheza mara kwa mara ni lazima aonyesha utayari wa kimwili na kiakili kwani bila ya mambo hayo muhimu ni vigumu kufanya vizuri uwanjani.

"Kila mchezaji ana nafasi ya kuonyesha uwezo wake ila kwa kuzungumzia suala la Okrah ninachojua ni majeruhi, sasa binafsi siwezi kuzungumzia mtu ambaye hayuko fiti kwa asilimia 100," alisema Robertinho na kuongeza;

"Nitafanya kazi na wachezaji ambao wapo tayari kujitoa kwa ajili ya kuipigania timu kwa sababu nina jopo kubwa la nyota wazuri na bora ninaoamini kwa pamoja tukishirikiana tunauwezo wa kufika mbali," alisema.

Kauli ya Mbrazili huyo inakuja baada ya taarifa kudai kwamba Okrah amekuwa anagombana na wachezaji wenzake mara kwa mara hali ambayo inamfanya kutopewa nafasi ya kucheza licha ya kuripotiwa anasumbuliwa na majeraha.

Kiongozi mmoja wa klabu hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina aliliambia Mwanaspoti kwamba baada ya mchezo wao na KMC uliopigwa Desemba 26 mwaka jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Okrah alimtishia Henock Inonga lakini Mkongo huyo akamkamata na kupiga vibao na kuondoka zake.

"Amekuwa na mambo mengi nje ya uwanja ndiyo maana tunaona kwa siku za hivi karibuni kiwango chake kimekuwa kinashuka kwa kasi, ni mlevi wa kupindukia hali inayompelekea kugombana na wenzake kila mara," kilisema chanzo chetu.

Kabla ya kujiunga na Simba msimu huu akitokea klabu ya Bechem United ya kwao Ghana, inaelezwa alimpiga kichwa mwamuzi msaidizi katika mchezo wa mwisho baada tu ya kukataa bao lake kwa madai kwamba aliotea jambo ambalo hakukubaliana nalo.

Hata hivyo, Mwanaspoti lilipomtafuta Okrah alikanusha vikali taarifa hizo huku akidai huko myuma alikuwa anakosekana kutokana na majeraha na muda siyo mrefu atarejea kwa ajili ya kuipambania timu yake ili iweze kufanya vizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live