Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho alikuwa anatafutiwa sababu - Yahya Njenge

Robertinho Alikuwa Anatafutiwa Sababu   Robertinho Robertinho alikuwa anatafutiwa sababu - Yahya Njenge

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Yahya Njenge amesema aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' alikuwa anatafutiwa sababu ya kufukuzwa na ikapatikana baada ya kufungwa na Yanga SC.

Yahya amesema, masiha ya Robertinho yalikuwa mashakani muda mrefu.

“Maisha ya Simba na Robertinho yalikuwa mashakani, ni kama walikuwa wanatafuta wapi atadondoka wamfute kazi

“Ukiangalia aina ya timu ambayo amepoteza dhidi yao (Yanga) ni timu yenye ubora na daraja la juu, mimi naamini alikuwa anatengenezewa namna yakuondoshwa.

“Hadi tunaona leo anaondoshwa huu ni mchakato wa muda mrefu na sababu imepatikana lakini siamini kama ndio tiba ya matatizo ya Simba," alisema Yahya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live