Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho ahamishia pira la Kibrazil Simba

Robertinho  Instagram Robertinho ahamishia pira la Kibrazil Simba

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' amesema yeye ni kocha kutoka Brazil hivyo anapenda wachezaji wake wacheze soka safi na kupata ushindi.

Robertinho aliyasema hayo jana Agosti 20, 2023 mara baada ya kumalizika kwa mechi yake dhidi ya Dodoma Jiji na kupata ushindi wa 2-0.

Alisema soka ni sanaa na ufundi hivyo anapenda wachezaji wake wacheze soka la kuvutia.

"Soka ni sanaa na ufundi, na mimi napenda soka la kushambulia. Simba ni timu kubwa na inataka ushindi kila siku, nawashukuru wachezaji wangu leo wamecheza vizuri na kupata matokeo," alisema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live