Wakati Simba ikilala macho kujua watakutana na nani katika hatua inayofuata ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Roberto Oliviera "Robertinho" yeye hana wasiwasi kwa kuwa tayari ameshaandaa mpango kazi wa namna ya kucheza michezo hiyo.
Akizungumza Robertinho amesema;
“Hizi mechi za hatua ya robo tutabadilika kidogo, unajua kama tutaanzia nyumbani kisha kwenda ugenini basi tunatakiwa kumaliza kazi hapa halafu utajua ucheze vipi kule ugenini, kwa hiyo kifupi tutakuja na sapraizi nyingine.”
“Nilisema awali Simba haina sababu ya kuhofia mpinzani yoyote, mimi ni kocha ambaye napenda presha ya mechi kubwa kama hizi. Hatukushinda dhidi ya Horoya kwa kubahatisha tulikaa na kuwasoma wapinzani wetu na kuwabadilishia mbinu zetu tofauti na tulivyocheza kwao,”
“Hata hizo mechi zinazokuja Simba itakuja na mkakati sahihi kulingana na timu tutakayopangiwa lakini kwa sasa tutawaangalia kwanza Raja ambao tunakwenda kukutana nao kumalizia mechi za makundi.”