Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Yanga waje tu

Robertinho Hgs.jpeg Kocha Mkuu mpya wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho'

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Simba jana kilikuwa Uwanja wa Highland Estate kuvaana na Ihefu katika mechi ya Ligi Kuu Bara na kuichapa mabao 2-0, ikiwa ni siku chache tangu iliichape mabao 5-1 kwenye robo fainali ya Kombe la ASFC, lakini kocha wao Roberto Olivieira 'Robertinho anajua Aprili 16 atakutana na watani zao Yanga na fasta ametoa tamko akiwatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo.

Kocha huyo raia wa Brazili, alisema kama kuna kitu anapenda basi ni mechi kubwa kama hizo na wala hana wasiwasi na kikosi alichonacho kwa ajili ya pambano hilo litakalokuwa la 110 tangu kuasisiwa kwa Ligi ya Bara mnamo mwaka 1965.

Robertinho alisema anamalizana kwanza na Ihefu, lakini akili zote zipo kwenye pambano la watani ambalo ni kama mtego kwao, kwani ikipoteza basi itakuwa imegeuzwa ngazi na vinara hao kwenda kutwaa taji kwa mara ya pili mfululizo.

Mechi hiyo ya watani itakuwa ni ya kwanza kwa Robertinho akiwa na Simba, huku ikikumbukwa kocha huyo amewahi kukutana na Yanga katika mechi ya kirafiki katika kilele cha Wiki ya Mwananchi alipokuwa akiinoa Vipers ya Uganda na kuwatoa nishai wenyeji kwa mabao 2-0.

Robertinho alisema anaiheshimu Yanga, lakini kamwe hawezi kuingia presha ya mchezo huo na kwamba anausubiri kwa hamu ili timu yake ionyeshe ubora wake.

"Presha juu ya Yanga? Hapana siwezi kuwa na hali hiyo kabisa kwanza mimi napenda mechi kama hizi ambazo mashabiki wanajaa uwanjani na kuwa na msisimkjo mkubwa, nimeshashinda mechi kubwa katika Uwanja kama Mracana kule kwetu Brazil ukiwa umejaa," alisema Robertinho na kuongeza;

"Tunaiheshimu Yanga lakini hata sisi tunaitaka hii mechi ili tuthibitishe ubora wetu mbele ya mashabiki wetu jambo zuri imekaa sehemu nzuri kwani kama tukishinda basi tutakuwa tumefanya maandalizi mazuri kwa morali kuelekea mechi ijayo ya kimataifa dhidi ya Wydad Casablanca."

Robertinho alisema anafahamu Yanga inaongoza ligi kwa muda mrefu, pia ina wachezaji bora na makocha wazuri, lakini anaamini mchezo huo utaamuliwa na timu itakayoingia na mbinu bora dhidi ya mwenzake.

"Kila mchezo una mpango wake hiyo itakuwa ni mechi tofauti na nyingine kwa timu ambayo itaingia na mbinu bora dhidi ya mwenzake itashinda, Simba ni timu kubwa itaingia kwa ubora mkubwa katika mechi kama hiyo."

Katika mchezo uliopita baina ya timu hizo zilipokutana kwenye ligi duru la kwanza matokeo yalikuwa 0-0, Simba ikitangulia kwa bao na Augustine Okrah na Stephane Aziz KI timu zote zilimaliza kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Chanzo: Mwanaspoti