Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Tuna wachezaji hawako fiti

Robertinho  Instagram Kocha Robertinho.

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesikia kilio cha hivi karibuni cha mashabiki wa timu yake juu ya mambo mawili na kisha akatoa ahadi moja kuwa amekisikia na anakifanyia kazi.

Mashabiki wa Simba katika siku za hivi karibuni wameonekana kutofurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu hiyo kwenye Ngao ya Jamii ambayo walitwaa huko Tanga wiki hii lakini pia kitendo cha baadhi ya nyota wake kutopangwa.

Akizungumza leo Agosti 16 mkoani Morogoro, Robertinho amesema mambo yote mawili ameyapokea na yatafanyiwa kazi hivyo mashabiki hawapaswi kuwa na wasiwasi.

"Simba ni timu kubwa na mashabiki wamekuwa wakitupa sapoti kubwa. Staili yetu ni kucheza soka la kuvutia na kushambulia muda wote. Hicho ndicho ambacho watu wakitegemee kutoka kwetu. Zilikuwa ni mechi mbili ngumu ambazo hata hivyo unaona tuliweza kucheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi. Naamini tutakuwa bora zaidi," alisema Robertinho

Kuhusu kutowatumia baadhi ya wachezaji, Robertinho alisema kuwa ni suala la ufiti tu ambalo anaamini baada ya muda mfupi litabaki kuwa historia.

"Tuna makundi mawili ya wachezaji. Wale walio fiti na kuna ambao bado hawajawa fiti kiasi cha kuwa na utayari wa kuwatumia kwa asilimia 100. Hivyo jukumu tulilonalo ni kutengeneza balansi nzuri baina yao. Wote ni wazuri na kila mmoja atacheza ukizingatia tuna mashindano mengi na hawapishani sana jambo la muhimu ni utimamu wa kiakili kwa kila mmoja kujua yuko timu kubwa," alisema Robertinho.

Akizungumzia mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Robertinho alisema wana imani watafanya vizuri.

"Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini Simba ni timu kubwa tunahitajika kupata ushindi na kuonyesha mchezo mzuri. Ushindi katika mechi ya kwanza ni jambo zuri katika kuanza safari ya kutimiza malengo yetu.

"Tutaendelea kucheza soka la kushambulia kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote," alisema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: