Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Sisi sio timu nyepesi wala sio wa kutudharau

Robertinho Mkwara Kocha wa Simba, Mbrazili Roberto Oliveira ‘Robertinho’

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kila mtu akiwa haiamini Simba kama ina uwezo wa kupata matokeo mbele ya Mabingwa watetezi Wydad Casablanca mechi ya Mkondo wa pili.

Kocha wa Simba SC, Roberto Oliviera "Robertinho" amesema kuwa watu wanakosea wanapoinyima nafasi Simba mbele ya wydad kwa kuwa waosio timu ndogo wala dhaifu kama wengi wanavyodhani.

Simba ambao wako safarini kuifata Wydad wanahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu kwa hatua ya Nusu Fainali kwani waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akizungumza wakati wakijiandaa na Safari ya Morocco Robertinho anasema;

“Sisi sio timu nyepesi tena watu watuheshimu tunaweza kwenda ugenini na tukafanya kitu, tunawaheshimu Wydad lakini hatutakwenda kinyonge pale Casablanca tutakwenda kupigania heshima ya klabu hii kubwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live