Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo 'Robertinho' raia wa Brazil amesema kuwa aliwabadilishia mbinu wapinzani wake Power Dynamos ya Zambia kwenye mchezo wa kirafiki wa Simba Day jana Agosti 6, 2023.
Robertinho amesema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambapo Simba wakiwa katika Dimba la nyumbani, Kwa Mkapa waliibuka na ushindi wa bao 2-0.
"Wachezaji wangu wamecheza vizuri, malengo yangu ni kuwa Bingwa msimu huu. Kwa sasa tuna wachezaji wa daraja la juu kwenye kikosi chetu. Nimetumia mpango tofauti kpindi cha kwanza kisha nikabadilisha mpango kipindi cha pili.
"Kipindi cha kwanza nimecheza kwa kushambulia zaidi kila wakati, kipindi cha pili nikacheza kwa kukaba na kushambulia mara chache. Hivi ndivyo navyotaka timu yangu iwe, tuendane na mifumo tofauti kulingana na mpinzani tunayekutana naye ili tufikie malengo yetu," amesema Kocha Robertinho.
Katika mchezo huo, Robertinho hakuanza na mshambuliaji kwenye kikosi chake;
Ally Salim
Shomary Kapombe
Mohamed Hussein
Henock Inonga
Che Malone
Sadio Kanoute
Leandrew Onana
Clatous Chama
Kibu Denis
Saido Ntibazonkiza
Mzamiru Yasin.
Baadaye aliwaingiza Jean Baleke, Fabrice Ngoma, John Bocco, Luis Miquissone kwa nyakati tofauti.