Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Kitanuka, ishu ya usajili wa Makusu ipo hivi

Kibu Robertinho.jpeg Kocha Robertinho na Kibu Denis

Sun, 15 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha pekee Mkuu Mbrazili kwenye Ligi Kuu Bara, Oliviera Robertinho amesema timu yake ya Simba baada ya kucheza na CSK Moscow kesho Jumapili, itapaa siku inayofuata na Jumanne itakinukisha na Mbeya City kwenye Uwanja wa Mkapa. Lakini inadaiwa mechi hiyo imesogezwa hadi Jumatano.

Simba juzi jioni ilicheza mechi ya kirafiki Dubai dhidi ya Al Dhafra. “Wachezaji watapumzika na hata siku ya mechi ya Jumapili watapata muda wa kupumzika kwani mchezo utakuwa jioni kwa hiyo naimani hakutakuwa na athari kubwa kwani hata muda wa kusafiri si mrefu kutoka Dubai kufika Tanzania,” alisema Robertinho huku kukiwa na tetesi viongozi walipanga kuomba mechi hiyo isogezwe mbele.

“Kambi hii ina faida kwa upande wetu nimepata muda wa kuwafahamu wachezaji vya kutosha pamoja na wasaidizi wangu, naimani kwa kushirikiana kwa pamoja tutakwenda kufanya vizuri kama malengo yetu yalivyo,”

“Tulikuwa kwenye eneo lenye kila kitu cha kufanyia mazoezi kama nilivyohitaji, utulivu ulikuwa mkubwa na wachezaji licha ya kuwa na muda mchache wameshika kwa kiasi kikubwa vile nilivyokuwa nawaelekeza.

“Hata hizi mechi mbili za kirafiki zinafaida kwetu kwani nitafahamu nilivyo waelekeza wachezaji kwa kiasi gani wamevifanya uwanjani kabla ya mechi za mashindano, uzuri hapa Simba nimekutana na nyota wengi wenye vipaji na uwezo wa kujituma.”

Kwenye usajili, uongozi Jumapili utakuwa umetangaza majembe mawili mapya ambayo ni mshambuliaji, Juan Makusu aliyevunjiwa mkataba wake na FC Lupopo na kiungo Ismael Sawadogo anayemaliza mkataba na Difaa El Jadida ya Morocco. Sawadogo ataanza mazoezi na Simba baada ya kutambulishwa huku timu hiyo itatokea kucheza dhidi ya Mbeya City Januari 17 au 18, Uwanja wa Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live