Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Kila mchezaji atacheza

Roberto Robertinho.jpeg Robertinho.

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazili Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameibuka na kutamka kuwa bado hana kikosi cha kwanza.

Kauli hiyo ameitoa wakati timu hiyo, imetoka kupata ushindi wa michezo miwili ya Ligi Kuu Bara waliyoipata msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Simba ilipata ushindi wake wa kwanza wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar 3-2 kabla ya kuifunga Dodoma Jiji 4-0.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Robertinho alisema kuwa bado kila mchezaji ana nafasi ya kuanza katika kikosi chake cha kwanza.

Robertino alisema kuwa, amefanya hivyo kwa lengo la kila mmoja kujituma na kuipambania timu ili wapate matokeo mazuri ya ushindi.

Aliongeza kuwa ataendelea kufanya mabadiliko ya kikosi cha kwanza katika kila mchezo unaofuatia hadi atakapopata kikosi cha kwanza kitakachopata matokeo mazuri.

“Nitaendelea kufanya mabadiliko ya kikosi changu cha kwanza katika kila mchezo hadi nitakapopata kikosi cha kwanza.

“Ni muda wa kila mchezaji hivi sasa kunionyeshea uwanjani kila atakapopata nafasi ya kucheza katika michezo ijayo ya ligi na kimataifa.

“Kikubwa ninataka kuwa na timu imara itakayotupa matokeo mazuri ya ushindi, ninaamini hilo litawezekana,” alisema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live