Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rivers kinyonge yawataja Yanga

Ukata Rivers United Rivers kinyonge yawataja Yanga

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutua nchini jana alfajiri, Kocha mkuu wa Rivers United, Stanley Eguma amesema kuwa anatambua ubora wa Yanga kuelekea katika mchezo wao wa marudiano lakini watapambana kupata matokeo ugenini.

Rivers United jana Ijumaa alfajiri walitua nchini wakitokea kwao Nigeria tayari kwa ajili ya mchezo wao marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya robo fainali unaotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Mkapa, kesho Jumapili.

Rivers wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na mlima mrefu mbele ya Yanga wa kufungwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Nigeria, hivyo waweze kusonga mbele wanatakiwa kushinda zaidi ya mabao mawili.

Akizungumza nasi, Kocha Eguma alisema kuwa wamekuja Tanzania kucheza na timu ambayo wanatambua kuwa ni bora na wanaamini kuwa watakutana na upinzani mgumu huku akisema kuwa licha ya yote lakini watahakikisha wanapata matokeo mazuri.

“Tunafahamu na kuutambua ubora wa wapinzani wetu Yanga, kwanza tuwapongeze kwa kufanikiwa kupata ushindi ugenini kwa maana ya Nigeria, tumekuja hapa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kama ambavyo wao walifanikiwa.

“Haina maana kwa kuwa tulifungwa kwetu basi tuje hapa kwa unyonge kwamba tutapoteza mchezo, hapana mpira haupo hivyo. Tutahakikisha kuwa tunaonyesha ubora wetu ili tujiweke katika mazingira mazuri ya kupata matokeo,” alimaliza kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live