Klabu ya Rivers United wameomba mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Yanga upigwe katika uwanja wao wa nyumbani, Adokiye Amaesimaka.
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limefanya ukaguzi wa uwanja huo baada ya kufanyiwa ukarabati na sasa wanasubiri majibu kutoka CAF.
Rivers United hawakutumia uwanja huo katika mechi zao za hatua ya makundi baada ya kuzuiwa na CAF ukiwa umekosa vigezo.
Mchezo wa mkondo wa kwanza kati ya Rivers United dhidi ya Yanga utapigwa Jumapili Aprili 23 huko Nigeria na marudiano kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Aprili 30.
Yanga imepania kupata ushindi wa jumla katika mechi zote mbili na kutinga nusu fainali.