Shabiki wa Wolves Jamie Arnold, 32, kutoka Norton Bridge huko Staffordshire amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kutokana na kumfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi beki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand.
Shabiki huyo pia amefungiwa kwa miaka saba kujihusisha na shughuli za mpira ndani na nje ya nchi
Ferdinand alifanyiwa ishara hizo Mei 23, 2021 baada ya kushangilia bao la Manchester United dhidi ya Wolves akiwa kama mchambuzi wa zamu ndani ya BT Sport, huku mechi hiyo ikimalizika kwa Wolves kufungwa mabao 2-1 katika uwanja wao wa nyumbani.
Mchezo huo ulikuwa ni wa kwanza kwa mashabiki kurejea uwanjani baada ya vikwazo vya coronavirus kuondolewa.
Hukumu hii ndiyo hukumu kali zaidi kuwahi kutolewa kwa shabiki wa soka aliyepatikana na hatia ya unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi kwenye mechi za mpira wa miguu.