Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rio amkataa Arnold, ampa sifa Reece James

Reece X Trent .jpeg Reece James x Trent Alexander Arnold

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa soka, Rio Ferdinand amesisitiza beki anayekipiga Chelsea, Reece James ni zaidi ya Trent Alexander-Arnold licha kufunga kwenye mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya wakati Liverpool ilipoilaza Rangers 2-0 Jumanne usiku na kuzidisha presha kwa kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate.

Ferdinand alisema hayo baada ya Reece kuonyesha kiwango safi kwenye mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya, lakini akasisitiza mabeki hawa wameleta ushindani mkubwa wa nani anastahili kuitwa katika kikosi cha England cha kwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia mwezi ujao.

James alihusika katika mabao mawili akifunga moja na kutoa asisti moja kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Milan kati kati ya wiki iliyopita.

Akizungumza kupitia kituo cha televisheni BT Sports, Ferdinand alisema kuna uwezekano James akaitwa kwenye kikosi cha England badala ya Trent Alexander.

“Naamini James ni bora zaidi ya Trent, hususan ukabaji wake, ana stamina ya hali ya juu, hii ni tofauti kubwa kati yao, upinzani unaleta ushindani, hii inasaidia sana wachezaji kuongeza bidii, jicho langu naona James anastahili zaidi, kwa upande wa Trent ataibuka na kurudi kwa ubora wake bado ni mchezaji mzuri,” alisema Ferdinand aliyetamba na timua ya taifa ya England enzi zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live