Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rio Ferdinand ateswa na kipigo cha Man City

Rio Ferdinand On Rio Ferdinand ateswa na kipigo cha Man City

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa Manchester United Rio Ferdinand amekiri kuwa tofauti ama pengo lililopo kati ya Manchester United na Manchester City ni kubwa kuliko alivyodhania.

Rio (43) amedai kuwa aliangalia mechi ya jana huku akiwa amejawa woga wakati upande wake wa zamani ukidhalilika kwa kipigo cha 6-3 ambacho alitania kuwa kilimfanya akajifiche kwenye handaki.

Kupitia mtandao wa Twitter Rio alishea jumbe mbalimbali wakati na baada ya mechi, baadhi ya jumbe hizo zilimaanisha: ”Nina alasiri iliyooza kama nini. Magroup ya WhatsApp yanawaka moto kwa sababu zote zisizo sahihi."

Pia, alitania kuwa ”Haaland hana heshima kwa hawa watetezi wa Ligi ya England."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live