Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rio Ferdinand asema Ten Hag haponi

Man Utd 'moja Ya Timu Zinazoburudisha' Ligi Ya Premia   Ten Hag Rio Ferdinand asema Ten Hag haponi

Tue, 21 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Rio Ferdinand anaamini Erik ten Hag atafutwa kazi Manchester United hata kama atasaidia timu hiyo kushinda taji la Kombe la FA msimu huu.

Man United itakipiga na mahasimu wao Manchester City kwenye fainali hiyo ya Kombe la FA, wikiendi hii.

Baada ya kumaliza nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, nafasi ya chini zaidi kuwahi kushikwa na timu hiyo kwenye ligi, hivyo kujipoza machungu hayo, Ten Hag na wachezaji wake watahakikisha wanashinda taji hilo la Kombe la FA katika fainali itakayopigwa Wembley.

Man United ikibeba taji hilo, itawasaidia kukata tiketi ya kucheza Europa League msimu ujao.

Hata hivyo, gwiji wa klabu hiyo, Ferdinand hashawishiki kama hilo litatosha kuokoa kibarua cha kocha Ten Hag, akisema:

“Kwa kadri ninavyotazama, kushinda au kushindwa, sioni kama Ten Hag ataendelea kuwapo kwenye timu msimu ujao. Sisemi ninachokitaka, nasema ninachoamini kinakwenda kutokea na naamini klabu itakwenda kutafuta kocha mwingine.

“Sidhani kama kushinda Kombe la FA kutabadili kitu chochote kwenye macho ya INEOS. Sijazungumza na mtu yeyote kwenye hiyo kampuni, nawaza tu, hicho ndicho ninachofikiri.”

Akizungumzia kiwango cha Man United kwa msimu huu, Ferdinand aliongeza:

“Weka majeruhi pembeni, kiwango cha timu kilikuwa kibaya sana. Timu nyingi zimekuwa na majeruhi, sawa pengine si kwa ukubwa kama wa Man United. Lakini, ukweli kiwango cha Man United kilishuka, kuanzia kwenye soka wanalocheza, halikuwa likitambulika kabisa ni la staili gani.”

Mmiliki mwenza wa Man United, bilionea Sir Jim Ratcliffe bado hajatangaza wazi kama anamsapoti Ten Hag, jambo linalozua utata wa kuhusu hatima ya Mdachi huyo huko Old Trafford.

Makocha wa zamani wa Chelsea, Graham Potter na Thomas Tuchel wamekuwa wakihusishwa na kibarua hicho cha kwenda kuchukua mikoba huko Old Trafford.

Chanzo: Mwanaspoti