Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rio Ferdinand ampakulia minyama Mainoo

Rio X Mainoo.jpeg Rio Ferdinand ampakulia minyama Mainoo

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa zamani wa klabu ya Manchester Rio Ferdinand amemsifu kiungo kinda wa klabu ya Man United Kobbie Mainoo ambaye alifanikiwa kuanza katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Everton.

Kiungo Kobbie Mainoo alicheza kwa kiwango bora sana katika mchezo dhidi ya Everton, Jambo ambalo limemuibua gwiji Rio Ferdinand na kumsifia kiungo huyo mwenye miaka 18 tu.

Beki huyo wa zamani wa Man United alisema hakumbuki mara ya mwisho kumuona kijana wa miaka 18 akicheza kwa kiwango kikubwa hivo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza, Huku akijaribu kuwagusia wachezaji kama Jack Wilshere na Cecs Fabrigas lakini akisisitiza Mainoo alikua bora zaidi juzi.

Kobbie Mainoo alianza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Everton, Huku akiwaacha wengi midomo wazi kutokana na ubora ambao alionesha kwenye mchezo huo licha ya umri wake mdogo wa miaka 18.

Mbali na kummwagia sifa Kobbie Mainoo lakini Rio Ferdinand alitoa tahadhari kijana huyo kaonesha ubora mkubwa kweli dhidi ya Everton, Lakini ni mchezo mmoja tu anahitajika kufanya hivi mara kwa mara ili kuendelea kuaminika zaidi na zaidi ndani ya klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live