Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rio Ferdinand: Wachezaji PSG wavivu

PSG VS NEWCASTLE Mastaa wa PSG

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa soka Rio Ferdinand ameiponda Paris Saint-Germain kutokana kiwango kibovu walichoonyesha katika mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Newcastle United Jumatano usiku kufuatia kichapo cha kushtukiza cha mabao 4-1.

Miguel Almiron, Dan Burn na Sean Longstaff walikuwa kinara katika mtanange huo uliyochezwa uwanja wa St James' Park kwani waliwidhalilisha miamba hiyo kutoka Ufaransa.

Lucas Hernandez alirudisha matumaini kwa PSG baada ya kufunga bao dakika ya 56, kabla ya Fabian Schar kuipa ushindi Newcastle dakika za mwisho.

Lakini Rio alishangazwa na matokeo hayo akidai wachezaji wa PSG ni wavivu kwa sababu hawakujituma dakika zote za mchezo.

"Dakika za mwanzo walionekana wapo vizuri, lakini hawakumlinda kipa wao na wakawapa nafasi Newcastle." alisema Ferdinand.

"Pointi kubwa waliruhusu bao dakika tatu na sekunde 20. Walicheza vibaya ndio maana mwisho wakaadhibiwa. Wachezaji walikuwa wavivu walishindwa kuwa makini na mechi. Tofauti kabisa unapowaangalia Newcastle, walikuwa makini dakika zote, wasumbufu, walitumia nguvu pia. Jinsi PSG ilivyotumia mfumo wa 4-2-4, kumpanga kati kiungo kinda (Warren Zaire-Emery) na kuchezesha wachezaji wanne mbele iliwagharimu." aliongeza

Matokeo hayo yanaifanya Newcastle kushika usukuni wa kundi baada ya kunyakuwa pointi nne katika mechi mbili. Katika mechi ya kwanza ya Ligi Mabingwa Ulaya vijana wa Eddie Howe waliilazimisha AC Milan sare ya 0-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live