Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rigobert Song akalia kuti kavu Cameroon

Rigobert Song. Rigobert Song.

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nigeria iliichapa Cameroon mabao 2-0 kwenye mchezo mwingine uliokuwa na mvuto wa hali ya juu na kumfanya kocha wa Simba Wasioshindika, Rigobert Song kuwa katika wakati mgumu.

Staa wa Nigeria, Ademola Lookman alifunga mabao yote mawili kwenye mchezo huo na kuipeleka timu yake kwenye robo fainali.

Nigeria inatafuta ubingwa wa nne wa michuano hiyo mwaka huu na itakuwa kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, Ijumaa kuivaa Angola.

Hata hivyo, kocha wa Cameroon, Rigobert Song anaweza kuwa na wakati mgumu zaidi kuliko makocha wote waliobaki na kuna hofu kuwa anaweza kuondolewa kwenye nafasi hiyo baada pia kushindwa kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia 2022.

Mashabiki wa Cameroon wanasubiri kuona uamuzi wa rais wa Chama cha Soka cha nchi hiyo, Samuel Eto’o, ambaye alikuwa akitazama mchezo huo akiwa jukwaani.

Mashabiki hao wamekuwa wakimlaumu Eto’o kuwa anatumia urafiki wake na Song na kushindwa kumtimua hata kama timu hiyo imefanya vibaya.

Song ambaye alitwaa ubingwa wa Afcon mara mbili akiwa mchezaji wa Cameroon, amesema bado hajafanya uamuzi wa nini cha kufanya baada ya kutolewa Afcon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live