Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Richarlison atupiwa ndizi uwanjani

Richarlison Richarlison atupiwa ndizi uwanjani

Thu, 29 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Tottenham Richarlison de Andrade (25) jana alitupiwa vitu kadhaa ikiwemo ndizi baada ya kuifungia timu yake ya Brazil jijini Paris.

Vitu hivyo vilirushwa wakati akilishangilia goli katika mechi ya kirafiki ambapo Brazil ilishinda mabao 5-1 dhidi ya Tunisia.

Kupitia mtandao wa Twitter Richarlison aliandika kuwa; "Ubaguzi utaendelea, kila siku kila mahali, kama mamlaka zitaendelea kupiga kelele tu bila kuwaadhibu vikali wahusika."

Shirikisho la soka la Brazil (CBF) limesisitiza kuwa ubaguzi haukubaliki na watabaki katika msimamo huohuo huku Rais wa CBF Ednaldo Rodrigues akiongeza kuwa "Iwe ndani au nje ya uwanja, tabia za namna hiyo hazitovumiliwa."

Aidha, kwa upande mwingine, legendari wa Manchester United, Rio Ferdinand amesema; “Ubaguzi wa rangi sasa unachukuliwa kama kufagia chini ya kapeti tu. Hakuna anayepiga kelele za kutosha, sio wachezaji, sio vilabu, sio mashirika ambao wamesimama vya kutosha kupinga ubaguzi. Huu ni upuuzi.

Tottenham nao hawakuwa nyuma kulaani tukio alilofanyiwa mchezaji wao; "tumesikitishwa na kitendo cha ubaguzi alichofanyiwa Richarlison jana wakati wa mchezo kati ya Brazil na Tunisia. Jambo hili halikubaliki na halina nafasi katika soka. Tunasimama na wewe, Richy," waliandika Tottenham kupitia akaunti yao ya Twitter.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live