Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Richarlison "Arise and Shine Brother", muda wako huu

Richarlison Bei Tottenham 2022 23 1664041678 93172 Richarlison "Arise and Shine Brother", muda wako huu

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wanae kibao wakiamua kuingia kwenye kuuza madawa ya kulevya those days kule Nova Venecia, Espirito Santo Brazil, yeye aliamua kuuza chocolate na ice creams.

Kilikuwa kichekesho kwa rafiki zake na wakaona hayupo serious na maisha ambayo yalikuwa ni magumu sana.

Kiuhalisia ngada ina mkwanja kuliko ice cream na chocolate. Walimwambia aache kuwa msichana akaze kiume.

Kwenye mgongo wa Richarlison kuna tattoo kubwa 3, Ronaldo Nazario de Lima upande wa kushoto, Neymar Junior upande wa kulia - katikati ni yeye Richarlison Andrade.

Tattoo zina maana kubwa sana. Ni inspiration. Tattoo yenye sura yake inamaanisha anajikubali.

Wakati wengi wakiamini kuondoka kwa Harry Kane, Spurs watapata wakati mgumu kwenye eneo la ushambuliaji, mimi na Richarlison tunaamini ni muda wa kwenda kuweka alama kwenye mioyo ya mashabiki wa Spurs.

Ni muda wa kwenda kuonesha kwa nini jezi namba 9 ilikwenda kwa Richarlison Andrade. Ni muda wa kuianza mission aliyoisubiri kwa muda mrefu.

Ni muda wa kwenda kuwa namba 9 wa timu. Tangu asajiliwe hakuwahi kucheza kama mshambuliaji wa kati comfortably, huu ndio muda.

Andaeni macho yenu. It's time to arise and shine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live