Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Richard Arnold Kumrithi Ed Woodward Man Utd

Mrithi United Richard Arnold, anatazamiwa kuwa mrithi wa Ed woodward

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Richard Arnold anajiandaa kuchukua nafasi ya Ed Woodward kwenye klabu ya Manchester United ambaye alitangaza kuachia ngazi baada ya mpango wa Super League kushindikana ambapo yeye nae alikuwa miongoni mwa watu walioshiriki.

Nafasi ya Ed Woodward sasa imepata mtu wa kuiziba japo Richard ataanza na nafasi ya “CEO” kwenye viunga vya Old Trafford na kuwa mtu wa kwanza kushika nyadhifa hiyo tokea David Gill mwaka 2013 kuishika wadhifa huo, wakati Ed Woodward kwa sasa anashika nafasi ya makamu mwenyekiti.

Richard awali alishafanya kazi kama mkurugenzi kwenye makampuni kama InterVoice, Nasdaq kabla ya kufanya kazi kama mkurugenzi wa biashara kwenye klabu ya Man Utd, pia alipandishwa cheo na kuwa “Group Managing Director” mwaka 2013.

Woodward anaondoka Man Utd kwa sababu hakuweza kufanikiwa ndani ya uwanja japo aliweza kufanya usajiri wa pesa nyingi kwenye kikosi cha United kama Paul Pogba, Romelu Lukaku na Angel di Maria, Richard anakwenda kurithi kiti cha mtu ambaye waliweza kufanya kazi bega kwa bega kwa kipindi chote kwenye viunga vya Carrington Complex

Chanzo: www.tanzaniaweb.live