Baada ya wachezaji wake waandamizi kuandamwa na majeraha kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza Gareth Southgate amemteua kiungo wa kati wa taifa hilo na klabu ya Arsenal Declan Rice kuwa nahodha kwenye mchezo wa leo dhidi ya timu ya Taifa ya Ubelgiji.
"Ni heshima kubwa sana kwangu kuvaa kitambaa na kuingia Wembley kama nahodha kwenye mchezo wangu wa 50 nikiwa na timu ya Taifa" alisema Rice kwenye mkutano na wanahabari jana.
Rice anavaa kitmbaa hicho ambacho awali kilivaliwa na Jordan Henderson na Harry Kane ambaye kutokana na kukosekana kwake kilivaliwa na beki Kylie Walker ambaye aliumia mchezo uliopita dhidi ya Brazil.