Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rice: Bukayo Saka atatupa ubingwa 2023/24

Image 478 1140x640.png Decline Rice na Bukayo Saka

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: Dar24

Kiungo ghali wa Arsenal, Declan Rice amesema anataka kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England kwenye msimu wake wa kwanza akiwa na uzi wa The Gunners huku akiamini Bukayo Saka atahakikisha taji hilo la 2023-24 linatua kaskazini mwa jijini London.

Rice mwenye umri wa miaka 24, amejiunga na Arsenal kwa ada ya Pauni 105 milioni, hivyo anakwenda kucheza timu moja na Mwingereza mwenzake, Saka.

Kikosi hicho kwa sasa kipo kwenye mechi za kujipima nguvu huko Marekani na nahodha huyo wa zamani wa West Ham United, Rice tayari ameshaanza kuzoeana na wachezaji wenzake wapya huku akitambua kitu ambacho kocha Mikel Arteta anataka kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu England mwezi ujao.

Arsenal ilimaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, alama tano nyuma ya mabingwa Manchester City, licha ya kuongoza ligi hiyo kwa muda mrefu.

Rice anaamini ataisaidia Arsenal kukamilisha kile ambacho ilishindwa kukifanya msimu uliopita na mwenyewe anasema hivi: “Nasubiri kwa hamu! Wakati niliposaini nilizungumza na kocha na tulisimama uwanjani ndani ya boksi. Ni uwanja wa aina yake ni bahati kubwa kucheza soka mahali hapa.”

Rice amekuwa akikoshwa na mavitu ya Saka, akiamini winga huyo ataweza kuisaidia Arsenal kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2023-24.

Kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, kocha Mikel Arteta amefanya usajili wa mastaa watatu kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chake na kutumia zaidi ya Pauni 200 milioni katika usajili huo baada ya kuwanasa Rice, Kai Havertz na Jurren Timber.

Chanzo: Dar24