Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Riccardo Calafiori kimeeleweka Arsenal

Calfioriiiii Riccardo Calafiori kimeeleweka Arsenal

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal inakaribia kukamilisha uhamisho wa beki Riccardo Calafiori kutoka Bologna mwenye umri wa miaka 22 ambaye alionyesha kiwango bora katka fainali za Euro mwaka huu akiwa na Italia.

Inaripotiwa kwamba Arsenal imekubali kulipa kiasi cha Euro 45 milioni na kisha itaongeza kiasi cha Euro 50 milioni kwa Bologna siku za usoni kulingana na ufanisi na mchango wa mchezaji huyo klabuni.

Usajili huo ulikuwa ukamilike mapema mwezi huu lakini Bologna walionekana kusita kumuachia Calafiori aondoke kwa vile Arsenal haikuonekana kuwa tayari kutoka kiasi cha fedha ambacho kilikuwa kinahitajika na Bologna kwa ajili ya kumuuza beki huyo anayemudu pia kucheza nafasi ya beki wa kushoto.

Kocha wa Arsenal,Mikel Arteta anaamini kwamba Calafiori atasaidia kuiimarisha zaidi safu yake ya ulinzi msimu ujao baada ya kumaliza ikiwa kinara wa chati ya timu zilizoruhusu idadi ndogo ya mabao kwenye Ligi Kuu ya England.

Hata hivyo Calafiori atalazimika kufanya kazi ya ziada ili aweze kupata nafasi ya kucheza mbele ya William Saliba na Gabriel Magalhães ambao pacha yao imeonekana kuwa na uelewano

Kipaji cha Calafiori kiliibuliwa na AS Roma ambayo ilimpa nafasi katika kikosi chake cha vijana na mwaka 2020 ilimpatia rasmi nafasi katika kikosi cha wakubwa katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Juventus.

Chanzo: Mwanaspoti