Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rhino, Mbao FC uwanjani,

Rhin+fc+pic Rhino, Mbao FC uwanjani,

Mon, 12 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Yohana ChalleDar es Salaam. Michezo ya kwanza ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inamalizika leo kwa Rhino Rangers kucheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Hadi sasa timu zilizoshuka daraja zimeonekana kuanza ligi kwa kusuasua huku Lipuli pekee akiondoka na pointi tatu baada ya kuifunga Mawenzi Market mabao 2-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro juzi Jumamosi.

Wakati Lipuli ikiondoka na ushindi huo, Singida United ilichezea kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Geita Gold mchezo uliofanyika Uwanja wa Nyankumbu, Geita.

Mabao hayo yalifungwa na Venance Ludovick dakika ya 19 na 34 na kuiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya pili huku Fountain Gate ikiwa kileleni mwa msimamo baada ya kuichapa 3-0 Allince FC.

Katika michezo ya ufunguzi wa FDL iliishuhudia Ndanda iliyoshuka daraja nayo ikibanwa mbavu ya bao 1-1 na African Lyon katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ushindi huo wa Geita inayoongozwa na Kocha Fredy Felix ‘Minziro’ umekuwa mwendelezo mzuri wa msimu uliopita baada ya kufanikiwa kumaliza nafasi ya pili na kuishia hatua ya mtoano.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz