Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi zambeba Benzema kutwaa Ballon d'Or 2022

Benzema Ballon 1.jpeg Benzema akinyanyua tuzo yake ya Ballon d'Or

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Karim Benzema kutoka ametwaa Tuzo ya Mshindi wa Ballon D'or kwa mwaka 2022 baada ya kuwashinda Wachezaji wafuatao:

1. Karim Benzema

2. Sadio Mane

3. Kevin De Bruyne

4. Robert Lewandowski

5. Mohamed Salah

6. Kylian Mbappe

7. Thibault Courtois

8. Vinicius JR

9. Luka Modric

10 Erling Haaland



- Sadio Mane ameshinda Tuzo ya Socrates ambayo ni maalum kwa Mchezaji aliyefanya ubinadamu (kusaidia jamii,...) nje ya Uwanja. Tuzo hii ya Socrates imetolewa kwa mara kwanza na Mane ndiye Mchezaji wa kwanza kupewa Tuzo hii.

Mane ameshinda Tuzo hii baada ya kukisaidia Kijiji alichozaliwa kwa kuwajengea Hospitali, Shule, kuwapa mshahara Wanakijiji (maskini) na mengine mengi bila kusahau kuwalea Mtandao wa Simu wenye kasi ya 4G.

- Gavi (18) wa FC Barcelona ameshinda Tuzo ya Kopa ambayo hutolewa kwa Mchezaji mwenye umri mdogo aliyefanya vizuri.

- Alexia Putellas wa FC Barcelona ameshinda Tuzo ya Ballon D'or kwa upande wa Wanawake kwa mara nyingine tena baada ya mwaka jana kushinda.

- Robert Lewandowski (Barcelona) ameshinda Tuzo ya Gerd-Müller ambayo hupewa Mchezaji aliyefunga mabao mengi kwa mwaka.

- Thibaut Courtois (Real Madrid) ameshinda Tuzo ya Yachine ambayo hupewa kwa Golkipa bora wa mwaka.

- Klabu ya Manchester City imeshinda Tuzo ya klabu bora ya mwaka.

- Ikumbukwe kuwa Tuzo za mwaka huu zimefanyika kwa mara ya kwanza bila uwepo Cristiano Ronaldo na Leonel Messi kwenye "Top 10" tangu 2006.

- Karim Benzema ni Mchezaji wa Tano (5) kutoka katika Taifa la Ufaransa kushinda Ballon D'or baada ya:

1. Raymond Kopa (1958)

2. Michel Platini (1983, 1984, 1985)

3. Jean-Pierre Papin (1991)

4. Zinédine Zidane (1998).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live