Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi za kibabe zinazoishi EPL

Thierry Henry Arsenal Rekodi za kibabe zinazoishi EPL

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tumeona mambo mengi ndani ya Premier League, iliyoanza takribani miaka 30 iliyopita. Kumbuka mwaka 1992 ndiyo ilianza kuitwa Premier League.

Hapa kuna rekodi 19 ambazo mpaka sasa hazijavunjwa.

1. Mchezaji kufunga hat trick tatu katika mechi chache (8 – Erling Haaland - 2022/23)

2. Timu kucheza mechi nyingi mfululizo bila ya kupoteza (Mechi 49 – Arsenal – Mei 7, 2003 mpaka Oktoka 24, 2004)

3. Mchezaji aliyecheza mechi nyingi mfululizo (Mechi 310 – Brad Friedel – Agosti 14, 2004 mpaka Septemba 29, 2012)

4. Kukusanya pointi chache kwa msimu (Pointi 11 – Derby County msimu wa 2007/08)

5. Kupoteza mechi nyingi mfululizo (Mechi 20 – Sunderland – 2003 mpaka 2005)

6. Mchezaji mkubwa zaidi (John Burridge – Miaka 43, siku 162 akiwa Man City dhidi ya QPR, Mei 14, 1995)

7. Kubeba ubingwa kwa tofauti ndogo (Pointi 0, tofauti ya mabao 8 – Man City 2011/12)

8. Bao la mapema (Sekunde 7.69 – Shane Long akiwa Southampton vs Watford, Aprili 23, 2019)

9. Bingwa aliyekusanya pointi chache (Pointi 75 – Man United 1996/97)

10. Kucheza mechi nyingi mfululizo nyumbani bila kupoteza (Mechi 86 – Chelsea – Machi 20, 2004 mpaka Oktoba 5, 2008)

11. Mashabiki wachache kuingia uwanjani (3,039 - Wimbledon vs Everton – Januari 26, 1993)

12. Hat-trick ya mapema (Dakika 2, sekunde 56 – Sadio Mane akiwa Southampton vs Aston Villa, Mei 16, 2015)

13. Kipa kudaka muda mrefu bila kuruhusu bao (Dakika 1,113 – Edwin van der Sar akiwa Man United, Novemba 15, 2008 mpaka Februari 18, 2009)

14. Mchezaji kufunga misimu mingi mfululizo (Misimu 21 – Ryan Giggs – 1992/93 mpaka 2012/13)

15. Mabao mengi kufungwa na mchezaji kipindi kimoja (Mabao 5 – Jermain Defoe akiwa Tottenham vs Wigan Athletic, Novemba 22, 2009)

16. Kocha aliyedumu muda mrefu (Miaka 21 na siku 224 – Arsene Wenger – Arsenal – Oktoba 1, 1996 mpaka Mei 13, 2018)

17. Mchezaji kuifunga mfululizo timu moja (9 - Sadio Mane akiwa Liverpool vs Crystal Palace)

18. Timu kuruhusu mabao machache kwa msimu (Mabao 15 – Chelsea – 2004/05)

19. Bao la mapema kutokea benchi (Sekunde 6 – Nicklas Bendtner akiwa Arsenal vs Tottenham, Desemba 22, 2007).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live