Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi za Simba ni balaa

Chama Vs Jwaneng.jpeg Clatous Chota Chama.

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyie hamuogopi? Kule Chama, huku Aziz Ki, hapa Pacome, pembeni Maxi Nzengeli hatimaye yametimia waliyokuwa wanayasubiri Wananchi, Clatous Chama sasa ni rasmi mali ya Yanga.

Baada ya kutambulishwa Yanga, Chama anaingia kwenye orodha ya wachezaji waliowahi kucheza timu zote mbili, Simba na Yanga.

Amewahi kufanya hivyo Haruna Niyonzima, Amis Tambwe, Emmanuel Okwi, Kelvin Yondani, Juma Kaseja, Ivo Mapunda, Jonas Mkude,Gadiel Michael, Bernard Morrison na wengine wengi.

SAKATA LAKE HADI KUSHINDWANA NA SIMBA

Baada ya kurejea nchini akitokea kwao nchini Zambia, Chama aliitwa na Bosi Dubai ambako alikwenda kwa mazungumzo baada ya kufika Dubai Chama aliongeza Dau kutoka pesa aliyokuwa anaitaka hapo mwanzo na kutaka apewe dolla 350 sana na zaidi ya milioni 800 ili asaini Simba.

Chama pia alihitaji mshahara wa zaidi ya milioni 40 kwa mwezi ili asalie ndani ya Simba Mo Dewji na kamati yake wakaona anafanya hivyo kwa sababu ya ofa ambayo ipo mezani kwake ya kutoka Yanga.

Leo Clatous Chama ametambulisha kujiunga na Yanga kwa Dolla 350 sawa na zaidi ya milioni 820 za Kitanzania huku atakuwa akilipwa mshahara wa kiasi cha milioni 35 kwa mwezi mmoja na kuwa mchezaji wa pili anayelipwa pesa nyingi katika timu hiyo baada ya Azizi Ki.

TAKWIMU ZA CHAMA LIGI KUU AKIWA SIMBA

MECHI: 139

MAGOLI: 27

ASSISTS: 54

TAKWIMU ZA CHAMA CAF AKIWA SIMBA

MECHI: 44

MAGOLI:15

ASSISTS:6.

Chama anaondoka SIMBA baada ya kudumu kwa miaka mitano na nusu alijiunga SIMBA 2018 akitokea Power Dynamos ya Zambia.

Ilikuwa ni ndoto ya mashabiki na wapenzi wa Yanga kuona mchezaji huyo anavaa jezi yao na kukipiga mitaa ya Jangwani, na hatimaye ndoto imekuwa kweli msimu ujao 2024/25 Chama atasambaza pasi za upendo mitaa ya Jangwani.

Pembeni yake kutakuwa na Pacome, kule Maxi Nzengeli, huku Aziz Ki, huenda Yanga sasa ikazidi kufanya vizuri zaidi kwenye soka la ndani na la Kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live