Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford ameingia kwenye vitabu mbalimbali vya rekodi baada ya kufunga goli 1 na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya NottNottingham Forest kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Carabao usiku wa kuamkia leo Alhamisi Januari 26, 2023.
Rashford ni mchezaji wa kwanza wa Manchester United kufikisha magoli 5 kwenye kombe la Carabao tangi Carlos Tevez afanye hivyo mwaka 2008-09.
Vile vile Rashford ndiye mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi (10) tangu kumalizika kwa mashindano makubwa duniani ya Kombe la Dunia yaliyopigwa Qatar mwezi Novemba hadi Desemba 18, 2022.