Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi za Musonda kimataifa zinatisha

Yanga Musonda010 Mshambuliaji wa Yanga, Keneddy Musonda.

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga, Keneddy Musonda amejiandikia rekodi yake ndani ya timu hiyo kwenye michuano ya kimataifa baada ya kuhusika kwenye mabao 11 tangu amejiunga na timu hiyo.

Musonda alijiunga na Yanga msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili na takwimu zake zinaonyesha amecheza mechi 17 na kuhusika kwenye mabao 11.

Kwa mujibu wa mtandao wa Yanga wameweka rekodi hizo na kubainisha msimu uliopita amecheza mechi tisa akifunga mabao matatu na kutoa pasi zilizozaa mabao tatu timu yake ikifika hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Msimu huu akiwa na timu hiyo amecheza mechi nane akifunga mabao matatu na kutoa asisti mbili.

Msimu huu Yanga imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali na ikiwa kundi D akiwa sambamba na Al Ahly ambaye anaongoza kundi kwa pointi 13, CR Belouizdad ambaye amemaliza nafasi ya tatu na Medeama ambayo imeburuza mkia.

Yanga sasa inasubiri itakutana na nani hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, katika droo itakayochezeshwa Machi 12, 2024 huko Cairo, Misri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: