Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi za Metacha zamkosha Kim Poulsen

Metacha Mnata Of Yanga Sc And John Bocco Of Simba Sc 19rxdtqigmuui1t01sugm4vmkh Metacha Mnata akionyesha uhodari wake

Thu, 19 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hii leo Kocha wa Timu ya Taifa "Taifa Stars", ameita kikosi cha wachezaji 28, ambao wataingia kambini kujiandaa kwa michezo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo na Madagascar.

Katika majina ya walioitwa yumo golikipa Metacha Mnata ambaye hana timu kwa sasa baada ya kutemwa na Yanga. wengi wameshangazwa na kitendo hicho. Kocha Poulsen ni mtazamaji na mfuatiliaji mzuri tu wa Ligi yetu na kama kocha ndio sehemu ambayo anaona Wachezaji wa Timu ya Taifa.

Hizi hapa rekodi za Metacha zilizomshawishi Kim amjumuishe nyanda huyo kwenye kikosi chake.

Ni mechi 23 ambazo alicheza alikuwa ni chaguo namba moja kwa makocha ambao walipita Yanga. Zama za Cedrick Kaze na sasa alimaliza na Nasreddine Nabi ambaye ni muumini mzuri katika suala la nidhamu.

Mnata katika mechi hizo alicheza dakika 2,070 aliruhusu mabao 13 ya kufungwa.

Ana wastani wa kuruhusu goli kila baada ya dakika 159.

Kipa huyo mzawa ana wastani wa kuokota nyavuni bao moja kila baada ya dakika 159 katika mechi ambazo amecheza jambo linaloonyesha kwamba uwezo kwenye mikono yake ni mkubwa.

Amekusanya jumla ya clean sheet 13 na alifungwa katika mechi 10 ndani ya ligi msimu wa 2020/21.

Timu ya Yanga ilimaliza msimu ikiwa nafasi ya pili na msimu ujao wa 2021/22 itashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika bila uwepo wa mikono ya nyota huyo.

Hapa alikuwa shujaa

Yanga 1-0 Mbeya City, Kagera Sugar 0-1 Yanga, Mtibwa Sugar 0-1 Yanga, Yanga 3-0 Coastal Union, Yanga 1-0 Polisi Tanzania, Biashara 0-1 Yanga, Gwambina 0-0 Yanga, Azam 0-1 Yanga, Yanga 1-0 JKT Tanzania, Mwadui 0-5 Yanga, Ihefu 0-3 Yanga. Namungo 0-0 Yanga na JKT Tanzania 0-2 Yanga.

Mechi ambazo alikumbana na misuko suko.

Tanzania Prisons 1-1 Yanga, Mbeya City 1-1 Yanga, Kagera Sugar 3-3 Yanga, Yanga 3-1 Dodoma Jiji, Yanga 2-1 Ruvu Shooting, Yanga 1-1 Simba, Yanga 1-1 Namungo, KMC 1-2 Yanga, Polisi Tanzania 1-1 Yanga, Ruvu Shooting 2-3 Yanga

Utata ulianzia hapa

Juni 17 aliweka mkataba wake rehani baada ya uongozi wa Yanga kumsimamisha kwa muda usiojulikana kutokana na kitendo chake kisicho cha kiuungwana kwa mashabiki ambao walikuwa wakimzomea kwa kueleza kwamba alifanya uzembe katika kuokoa bao la pili ambalo lilifungwa na David Richard, dakika ya 82.

Mapema nwezi huu Metacha aliachwa na Yanga na huenda mechi hizo za timu ya Taifa ndizo zikawa sababu ya kumpa dili nono.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live