Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi za Mamelodi alipokutana na Yanga, kumbe Wananchi wanamuweza

Mamelodi Yanga Sz Mamelodi na Yanga

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Masandawana kutoka Bondeni Afrika Kusini Mamelodi Sundowns FC wamepangwa na Yanga katika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itachezwa kati ya Machi 29, 30 ama 31, 2024.

Moja kati ya kitu cha kujikumbusha ni namna ambavyo Mamelodi Sundowns walitoa wachezaji wengi katika Afcon 2023 iliyomalizika kule nchini Ivory Coast.

Pichani hapo juu (kulia) ni wachezaji 11 wa Mamelodi Sundowns ambao waliitwa timu ya Taifa ya Afrika Kusini pamoja na Namibia. Pia mlinda mlango Ronwen Williams aliibuka kipa bora ya mashindano ya Afcon 2023.

Jumapili ya Mei 27, 2001, kwenye michuano ya CAFCL hatua ya pili ya mtoano, Mameldoi alitoa sare ya bao 3-3 na Yanga katika Dimba la CCM Kirumba Stadium lakini mechi ya marudiano kule Afrika Kusini, Mamelodi aliibuka na ushindi wa bao 3-2, hivyo Mamelodi akasonga mbele.

Moja ya kitu ambacho inawezekana mashabiki wa soka wamesahau ni kwamba hawa Mamelodi Sundowns waliwahi kumfunga bao 5-1 CR Belouizdad hapa hapa kwa Mkapa.

Ilikuwa ni mechi ya hatua ya makundi ya CAFCL mnamo Febuari 28, 2021 hivyo Mamelodi Sundowns sio wageni wa kupata ushindi mnono katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Februari 1, 2017, wakiwa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, na wakiwa wameweka Kambi nchini Tanzania, kwa ajili ya Ligi Kuu nchini Afrika Kusini na mchezo wa Super Cup dhidi ya TP Mazembe, Mamelodi waliomba mechi ya kirafi na Azam FC ikiwa ya moto, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa (Mkapa Stadium kwa sasa) na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Kwa rekodi hizi za Mamelodi akiwa nchini Tanzania, je yanga atamfunga paka kengele?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: