Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi za Aziz Ki zinatisha

Aziz KI 9 Goals Aziz Ki

Sun, 11 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki ambaye huu ni msimu wake wa pili akivaa jezi ya Young Africans SC, tayari amevunja rekodi yake ya magoli katika Ligi Kuu ya NBC.

Aziz Ki raia wa Burkina Faso, alijiunga na Young Africans SC msimu wa 2022-2023 akitokea Klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Katika msimu wa kwanza 2022-2023 akiwa Young Africans SC, Aziz Ki alifunga magoli tisa ndani ya Ligi Kuu ya NBC baada ya timu yetu kucheza jumla ya mechi 30, huku akiwa na hat trick moja aliyoifunga dhidi ya Kagera Sugar, tuliposhinda magoli 5-0, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Msimu huu wa 2023-2024, tayari Aziz Ki amefunga magoli 10 ikiwa ni moja zaidi ya ilivyokuwa msimu mzima uliopita 2022-2023.

Magoli hayo 10 yanamfanya Aziz Ki kuwa kinara wa ufungaji katika ligi hiyo. Pia ana hat trick moja aliyoifunga dhidi ya Azam, tuliposhinda magoli 3-2 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mechi 16 zilizosalia ili kukamilisha msimu huu wa 2023-2024, Aziz Ki anaisaka rekodi mpya ya kufunga magoli mengi zaidi, ikiwezekana kuongeza hat trick.

Ukiachana na hilo, Aziz Ki tangu aanze kucheza Ligi Kuu ya NBC, amefanikiwa kufunga magoli 19, huku goli la kwanza akilifunga Septemba 13, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar, Young Africans SC ilishinda 3-0.

Rekodi zinaonesha kwamba, katika msimu wa 2022-2023 ambapo Aziz Ki alifunga magoli 9, alizifunga timu za Mtibwa Sugar (2), Simba (1), Azam (1), Namungo (1), Kagera Sugar (3) na Singida Big Stars (1).

Msimu huu wa 2023-2024, Aziz Ki amefunga magoli 10 dhidi ya timu hizi; KMC (1), JKT Tanzania (1), Geita Gold (1), Azam (3), Simba (1), Mtibwa Sugar (2) na Tabora United (1).

Timu iliyofungwa magoli mengi na Aziz Ki katika Ligi Kuu ni Mtibwa Sugar (4) na Azam (4), inafuatia Kagera Sugar (3), kisha Simba (2). Zilizobaki KMC, JKT Tanzania, Geita Gold, Tabora United, Namungo na Singida Big Stars, zenyewe zimefungwa goli mojamoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live