Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi ya misimu minne yamtesa kipa

Kipa Ken Golddd Rekodi ya misimu minne yamtesa kipa

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa KenGold, Castor Mhagama amesema huenda msimu huu akatimiza ndoto yake ya kupandisha timu Ligi Kuu aliyosotea kwa misimu minne mfululizo.

Nyota huyo amekuwa na kiwango bora msimu huu na hadi sasa anaongoza kwa kutoruhusu mabao 'Clean Sheets' katika mechi 14 kati ya 22.

Akizungumza na Mwanaspoti Mhagama alisema, siri kubwa ya mafanikio hayo ni kutokana na kujituma, kusikiliza na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi huku akieleza kila mchezaji ana kiu ya kuandika hostoria ya kuipandisha timu Ligi Kuu.

"Nimesota sana Championship kwa misimu minne sasa, timu nilizopitia nyingine sikuwa na uhakika wa kucheza mara kwa mara ila nashukuru hapa KenGold nimeaminiwa zaidi na ninahitajika kuonyesha uaminifu huo niliopewa," alisema na kuongeza;

"Huenda nikatimiza ndoto yangu ya muda mrefu kutokana na matokeo tuliyonayo, lazima tuendelee kupambana kutokana na vita ya kupanda Ligi Kuu Bara."

Nyota huyo wa zamani wa Mbeya Kwanza, Mbeya City, Kitayosce (Tabora United) na Ndanda FC, ndiye aliyecheza mechi nyingi akiwa na kikosi hicho na amecheza michezo 21 kati ya 22 na kuiweka usukani timu hiyo kwa kukusanya pointi zake 50.

Katika mechi hizo, kipa huyo ameruhusu mabao 10, huku akiwahi pia kuichezea Tunduru Korosho wakati inashiriki Ligi ya First League

Chanzo: Mwanaspoti