Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi tamu AFCON 2023

Algeria Squad Rekodi tamu AFCON 2023

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Rekodi. Zinawekwa na kuvunjwa. Kwenye Fainali za Afcon, kuna rekodi nyingi, nyingine zimeshavunjwa na nyingine ni za muda mrefu na hadi sasa hazijavunjwa.

Afcon 2023, zinatarajiwa kuanza Jumamosi Januari 13, Ivory Coast, huko, mastaa wanaenda kutafuta na kuvunja rekodi lakini kuna hizi ni za muda mrefu bado hazijavunjwa.

HAKUNA MGENI

Hakuna taifa linaloshiriki fainali hizi kwa mara ya kwanza. Nchi nzote Afrika zimeshiriki kwa nyakati tofauti.

UBABE

Misri ndio kinara wa kubeba taji la Afcon mara nyingi zaidi (10). Mara ya mwisho ilibeba mwaka 2010 na imewahi kubeba mara tatu mfululizo (2006, 2008 na 2010). Cameroon ni taifa la pili ikichukua mara tano.

MAKOCHA WABABE

Hassan Shehata wa Misri na Charles wa wanaoongoza kwa kuwa na mataji mengi na kila mmoja ameshinda mara tatu,

KUPOTEZA FAINALI MARA NYINGI

Katika fainali saba, timu ya taifa ya Ghana imeporeza fainali nne.

NAFASI YA TATU

Nigeria ndio inaongoza kwa kumaliza nafasi ya tatu mara nyingi (4), sawa na wenyeji wa michuano hiyo ya mwaka huu, Ivory Coast.

MFUNGAJI BORA

Lejendari wa Cameroon, Samuel Eto’o ambaye kwa sasa ni rais wa chama cha soka cha nchi hiyo, anashikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote kwenye fainali hizo (18) akifanya hivyo kwenye fgainali sita alizoichezea timu yake ya taifa.

MABAO MENGI KWA FAINALI MOJA

Hadi sasa Pierre Ndaye Mulamba mshambuliaji wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo anashikilia rekodi hii. Staa huyu aliyepewa jina la utani la Mutumbula ‘muuaji’, alifunga mabao tisa kwenye mashindano ya mwaka 1974 na hadi sasa hakuna aliyewahi kufanya hivyo.

BAO LA MAPEMA

Staa wa Misri, Ayman Mansour alifunga bao sekunde ya 23 ya mchezo dhidi ya Gabon, Mafarao wakishinda 4-0, kwenye fainali za mwaka 1994 na hadi sasa hakuna aliyemfika.

MFUNGAJI MWENYE UMRI MDOGO

Shiva N zigou wa Gabon anashikilia rekodi hii hadi sasa alipofunga bao mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 16 na siku 93, kwenye mechi dhidi ya Afrika Kusini.

MFUNGAJI MZEE

Ni Hossam Hassan kutoka Misri alifunga bao dhidi ya DR Congo akiwa na umri wa miaka 39 na siku 174.

MABAO MENGI MECHI MOJA

Laurent Pokou wa Ivory Coast alifunga mabao matano kwenye mashindano ya mwaka 1970 dhidi ya Ethiopia.

KIPA MFUNGAJI

Kennedy Mweene raia wa Zambia ndiye kipa pekee kuwahi kufunga bao kwenye mashindano haya, alifunga mwaka 2013 dhidi ya Nigeria.

MECHI NYINGI BILA KUFUNGWA

Misri iliwahi kucheza mechi 21 bila ya kufungwa kati ya mwaka 2008 hadi 2010, hakuna taifa lililowahi kufanya hivyo tena.

WALIOKULA CHUMVI

Ahmed Hassan (Misri) na Rigobert Song (Cameroon). wote wamecheza mara nane, kuanzia mwaka 1996 hadi 2010.

MARA MBILI

Mahmoud El-Gohary kutoka Misri ndiye wa kwanza kushinda taji kama mchezaji na baadae akiwa kocha kisha nyota wa Nigeria, Stephen Keshi.

KOCHA MGENI KUSHINDA

Mwaka 1959, Pal Titkos alikuwa kocha wa kwanza mgeni kushinda Afcon, akifanya hivyo na kikosi cha Misri, pia ndiyo ulikuwa ubingwa wa kwanza wa Misri.

KOCHA KUSHINDA MATAIFA MAWILI

Herve Renard alishinda taji akiwa na Zambia mwaka 2012 na Ivory Coast 2015.

MCHEZAJI MZEE KUCHEZA

Essam El-Hadary wa Misri alicheza Afcon mwaka 2017 na umri wa miaka 45.

MAHUDHURIO MAKUBWA

Mwaka 1986 mechi kati ya Misri na Cameroon iliyopigwa dimba la Cairo ilihudhuria na mashabiki 120,000, ndio inashikilia rekodi ya mashabiki wengi hadi sasa.

MABAO MENGI

Mabao tisa yalifungwa kwenye mechi kati ya Misri na Nigeria mwaka 1963. Hii pia ilikuwa mara ya kwanza timu hizi kukutana kwenye Afcon.

WENYEJI MABINGWA

Mara 11 wenyeji wa mashindano haya walifanikiwa kuwa mabingwa, wenyeji hao ni Misri, Ethiopia, Ghana, Nigeria, Afrika Kusini na Tunisia.

Miaka 20 iliyopita Ivory Coast ikiwa mwenyeji ilitolewa kwenye hatua ya makundi.

WAANDAJI MARA NYINGI

Misri imeandaa Afcon mara nyingi zaidi (5), kati ya hizo imebeba taji hilo mara tatu.

Chanzo: Mwanaspoti