Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi kumbeba Zahera kwa Ruvu Shooting leo

73249 Zahera+pic

Wed, 28 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya kufanikiwa kuivusha Yanga katika Ligi ya Mabingwa, kocha Mwinyi Zahera anatarajia kuchanga karata zake leo katika mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting huku rekodi za misimu miwili zikimbeba.

Yanga imeingia hatua ya pili ya mashindano hayo baada ya kuifunga Township Rollers bao 1-0 ugenini na sasa inatarajia kukutana na Zesco.

Yanga kabla haijakutana na timu hiyo leo itakuwa na mtihani wa kuhakikisha inapata matokeo ili kuendele kujihakikishia uaminifu kwa mashabiki wake ambao wanaimani na timu hiyo kutokana na kupata matokeo ugenini.

Zahera anabebwa na rekodi za misimu miwili mfululizo kutoka kwa Shooting baada ya msimu uliopita kupata matokeo ya mabao 3-2, Mabao yalifungwa na Amis Tambwe, Feisal Salum 'Tei Toto' na Herietir Makambo kwa upande wa Yanga, huku Fully Zulu Maganga na Saidi Dilunga kwa mkwaju wa penati wakifunga kwa Ruvu Shooting.

Wakati msimu wa mwaka 2017 waliibuka na ushindi wa bao 2-0 mabao yalifungwa na Saimon Msuva kwa penati na Obrey Chirwa kwa kichwa krosi ilichongwa na Msuva.

Makocha wa pende zote mbili wamesema wanatarajia mchezo mgumu lakini kila mmoja anahitaji matokeo kwa lengo la kuhakikisha anaanza vyema karata yake ya klwanza msimu huu.

Pia Soma

Zahera alisema haamini katika rekodi mpira unachezwa dakika tisini na ndio zitakazoamua matokeo huku akitamba kuwa anatarajia kupata matokeo kutokana na nyota wake kuwa katika hari ya mchezo.

Kocha wa Ruvu Shooting,Salum Mayanga alisema wanatarajia mchezo wa ushindani huku akibainisha kuwa dakika tisini ndio zitaamua matokeo.

Chanzo: mwananchi.co.tz