Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi, Takwimu Ligi Kuu raundi ya 22 katika namba

Bangala, Aucho N Mayele Rekodi, Takwimu Ligi Kuu raundi ya 22 katika namba

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zimebakia raundi nane tu kabla ya kutamatika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23 ambayo ipo kwenye raundi ya 22 sasa, jana kulikuwa na mechi moja tu ya raundi ya 23 kati ya Ihefu dhidi ya Singida United, huku michezo mingine ikitarajiwa kuendelea Ijumaa ijayo.

Wakati ligi ikiwa raundi ya 22, kuna rekodi nyingi na takwimu zimewekwa na wachezaji pamoja na timu 16 zinazoshiriki.

Katika makala haya tumekusanya takwimu na rekodi mbalimbali za ligi ambazo zimewekwa mpaka kufikia raundi ya 22 na kuziandika kwa mtindo wa namba...

59. Ni pointi inazomiliki Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ikiwa bado iko kileleni mwa msimamo.

54. Simba imepachika idadi hii ya mabao kwenye Ligi Kuu, ikiwa ndiyo timu iliyofunga mabao mengi zaidi mpaka sasa.

53. Hizi ni pointi za Simba ilizonazo mpaka sasa kwenye ligi na inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo huo.

43. Azam FC wana idadi hii ya pointi mpaka sasa kwenye Ligi Kuu, lakini Singida Big Stars ina idadi hii ya pointi, lakini zinaweza kubadilika baada ya mechi ya jana kati ya timu hiyo dhidi ya Ihefu.

41. Yanga wamefunga idadi hii ya mabao kwenye Ligi Kuu ambapo inakamata nafasi ya pili kwa kupachika mabao mengi baada ya Simba.

36. Hii ni idadi ya mabao walioyonayo Azam FC kwenye Ligi Kuu mpaka sasa, ikiwa ni timu inayoshika nafasi ya tatu kwa kuwa na mabao mengi.

32. Hii ni idadi ya mabao ambayo timu za Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar zimeruhusu kwenye nyavu zao, zikiwa ndiyo timu zilizoruhusu mabao mengi mpaka sasa. Polisi Tanzania kama ikiruhusu bao lolote leo iwe matokeo ya sare, kushinda au kufungwa dhidi ya Kagera Sugar, itaongoza kwa kupachikwa mabao mengi.

31. Ni pointi za Geita Gold ilizonazo mpaka sasa kwenye ligi, ikiwa kwenye nafasi ya tano ya msimamo.

30. Prisons inashika nafasi ya pili kwa kufungwa mabao mengi, ikiwa imeruhusu idadi hii ya mabao kwenye ligi mpaka sasa.

29. Baada ya kuibugiza Dodoma Jiji mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Mtibwa Sugar imevuna idadi hii ya pointi kwenye Ligi Kuu, ikiikuta Namungo FC ambayo ilibakiwa na idadi hii ya pointi baada ya kubugizwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, mechi iliyochezwa Februari 4.

28. Ni idadi ya mabao ambayo imeruhusu timu ya Coastal Union kwenye nyavu zao mpaka sasa.

27. Ni idadi ya mabao ambayo Dodoma Jiji wameruhusu mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa kwenye nafasi ya 11 na pointi zake 24.

26. Hii ni idadi ya pointi ilizonazo Kagera Sugar, ambayo inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi hiyo.

25. KMC na Ruvu Shooting wameruhusu idadi hii ya mabao kila moja kwenye Ligi Kuu mpaka kufikia raundi ya 22.

24. Hizi ni pointi za Dodoma Jiji na Mbeya City kwenye ligi, lakini Mbeya City ikiwa juu ya msimamo wa mwenzake kwenye nafasi ya 10 na Dodoma Jiji 11 kwa tofauti ya wingi wa mabao.

23. Ni pointi za KMC ilizonazo mpaka sasa kwenye ligi, ikiwa kwenye nafasi ya 12 ya msimamo.

22. Hii ni idadi ya raundi ambazo Ligi Kuu imefikia mpaka sasa, pia Prisons ina idadi kama hii ya pointi ikiwa kwenye nafasi ya 13.

21. Yalikuwa ni mabao ya kufunga ya Ihefu kabla ya mechi ya jana jioni dhidi ya Singida Big Stars, kama hawakupata bao lolote basi yanabaki yalivyo.

20. Haya ni mabao ya kufunga ya timu za KMC na Kagera Sugar zimefunga idadi hii kila moja.

19. Yanga wameshinda mara 19, ikiwa juu kileleni mwa msimamo mpaka sasa.

18. Ni mabao ya kufunga kwa timu za Prisons na Coastal Union zikiwa pia zinafuatana kwenye msimamo, Wajelajela wakishika nafasi ya 13 na Wanamangusi ya 14.

16. Hii ni dadi ya mechi ilizoshinda mpaka sasa ikiwa kwenye nafasi ya pili ya msimamo.

15. Fiston Mayele, straika wa Yanga amefunga idadi hii ya mabao na ndiye anayeongoza mpaka sasa kwenye ligi.

14. Ni idadi ya pasi za mwisho za kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama ambaye anaongoza kwa 'assist' mpaka sasa.

13. Namba hii inasimama kama idadi ya mechi ambazo kipa wa Yanga, Djigui Diarra amekaa langoni bila kuruhusu wavu wake kutikisika 'clean sheets'.

10. Haya ni mabao ambayo Yanga imeruhusu kwenye wavu wake, ikiwa ndiyo timu iliyosuruhu mabao machache zaidi mpaka sasa kwenye ligi.

9. Ni idadi ya mechi ilizopoteza Namungo kwenye Ligi Kuu mpaka sasa, ikiwa na pointi 29 kwa sasa.

8. Namba hii inasimama kwa timu ndugu, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar. Kila moja imepoteza idadi hii.

7. Dodoma Jiji, Mtibwa Sugar, Geita Gold, Mtibwa Sugar ni idadi ya mechi zilizoshinda.

6. Ni idadi ya penalti ambazo Dodoma Jiji imepata kwenye Ligi Kuu mpaka sasa, ikiwa ndiyo timu iliyozawadiwa matuta mengi zaidi mpaka sasa.

5. Mohamed Hussein 'Tshabalala' wa Simba ndiye beki anayeongoza kwa 'assist' kwenye Ligi Kuu, akiwa ametoa pasi za mwisho mara tano.

4. Ni idadi ya mechi za kushinda kwa timu za Ruvu Shooting na Coastal Union hadi kufikia raundi ya 22.

3. Polisi Tanzania ambayo inaburuza mkia, ndiyo timu pekee iliyoshinda mechi chache kwenye Ligi Kuu, ikishinda mara idadi hii.

2. Yanga na Ihefu zimetoka sare mara idadi hii kwenye ligi, zikiwa ni chache zaidi, lakini kwa Ihefu itaendelea na rekodi hii kama itafungwa au kushinda kwenye mechi yake dhidi ya Singida Big Stars iliyotarajiwa kuchezwa jana.

1. Yanga na watani zao, Simba, zimepoteza mechi chache zaidi kwenye ligi, kila moja ikipoteza mara moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live