Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi: Bila Maguire Man U hawatoboi

Rekodi: Bila Maguire Man U Hawatoboi Rekodi: Bila Maguire Man U hawatoboi

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

‘Rekodi’ zinaonesha kuwa ‘klabu’ ya Manchester United imekuwa ikishinda sana ‘mechi’ ambazo beki wao wa kati Harry Maguire akianza kwenye kikosi cha kwanza.

Kwa mujibu wa Sky Sports, inaeleza kuwa tangu October 22 mwaka jana katika ‘mechi’ 16 ambazo Man United ilianza ikiwa na beki huyo imeshinda ‘mechi’ 15, huku ‘mechi’ 44 ambazo ilianza bila ya mchezaji huyo ilishinda ‘mechi’ 22 tu.

Vilevile Man United huwa na asilimia 93 ya kushinda kwenye mchezo wakati mchezaji huyo anapokuwa uwanjani.

Kwa upande wa kuruhusu mabao Man United ina wastani wa 0.7 wa kuruhusu bao katika ‘mechi’ ambazo Maguire ameanza na zile ambazo hakuanza ni wastani wa 1.3.

Mchezaji huyo alisajiliwa na ‘timu’ hiyo mwaka 2019 akitokea ‘klabu’ ya Leicester City.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live