Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi 10 Ligi Kuu ambazo hazijavunjwa mpaka sasa

Yangasc Bingwa 30 Rekodi 10 Ligi Kuu ambazo hazijavunjwa mpaka sasa

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 inaelekea mwisho na baadhi ya rekodi ligi kuu Tanzania bara ambazo hazijavunjwa mpaka sasa.

1 » Tabora United inabaki kuwa timu pekee iliyoingia kwenye pitch kucheza mchezo wa ligi kuu ikiwa na wachezaji nane.

2 » Yanga SC inashikilia rekodi ya kushinda mabao (5) katika kila mchezo kwenye mechi (4) tofauti za ligi kuu katika msimu mmoja.

◉ 5 - 1 Simba SC ◉ 5 - 0 JKT Tanzania ◉ 5 - 0 KMC ◉ 5 - 0 Ihefu.

3 » Mchezaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein (Mmachinga) anaendelea kuwa mchezaji pekee aliyefunga mabao mengi (26) katika msimu mmoja.

4 » Mchezaji wa Yanga, Jonas Gerard Mkude anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye makombe mengi ya Ligi Kuu akiwa amechukua akiwa na timu mbili kubwa nchini, watani wa jadi Simba na Yanga kwa nyakati tofauti akiwa amechukua mara 6.

Mkude ametwaa mataji hayo kama ifuatavyo;

2011/12 2017/18 2018/19 2019/20 2020/21 2023/24.

5 » Yanga SC inashikilia rekodi ya kucheza michezo mingi mfululizo ligi kuu bila kupoteza 'UNBEATEN 49'.

6 » Simba SC inashikilia rekodi ya kutorejea uwanjani kipindi cha pili (Mpira kwapani) kwenye mechi ya Kariakoo derby baada ya kufungwa (3-0) na Yanga kipindi cha kwanza.

7 » Simba SC inashikilia rekodi ya kushinda mabao mengi (6) kuanzia ligi ilipoanzishwa (1964) kwenye mechi ya Kariakoo Derby.

8 » Yanga SC inashikilia rekodi ya kutwaa Ubingwa mara nyingi zaidi (×30) ligi kuu.

30 - Young Africans Sports Club. 22 - Simba Sports Club. 02 - Mtibwa sugar.

9 » Yanga wanashikilia rekodi ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu mara 4 back to back katika awamu (4) tofauti, wakikabidhiwa Ubingwa 23 | 24 itakuwa awamu ya (5).

◉ 1968 - 1969 - 1970 - 1971 - 1972 ◉ 1991 - 1992 - 1993 ◉ 1996 - 1997 - 1998 ◉ 2015 - 2016 - 2017 ◎ 2022 - 2023 - 2024.

10 » Yanga wanashikilia rekodi ya kumaliza katika nafasi (2) za juu ligi kuu Tanzania bara mara nyingi zaidi kuliko klabu yoyote.

Kuna baadhi ya misimu Yanga SC walikuwa hohehahe kiuchumi lakini wali-manege kumaliza msimu ndani ya top two (2).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live