Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Reinford Kalaba ameshinda kifo lakini Dunia inamsubiri

Kalaba Hosp Reinford Kalaba ameshinda kifo lakini Dunia inamsubiri

Sun, 5 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tufe la hofu juu ya mke wake lililokuwa linakaribia kuyeyuka kwenye moyo wa Boyd liliibuka tena. Safari hii likiwa zito zaidi na la moto zaidi. Lakini bado moto huo ulimletea ubaridi mkali uliomfanya azidi kutetemeka baada ya kusikia taarifa mbaya za ajali.

Alitamani kumuuliza mtu aliyempigia simu kumpa taarifa juu ya ajali ya mke wake. "usaliti huu umewezekana vipi" lakini aliishia kujisemea kimoyo moyo hapana. Boyd Alijisahihisha mwenyewe mara moja. Lisingekuwa swali la maana sana, badala yake aliuliza "wapo hai"

Taarifa ya kifo cha mke wake kilimfanya Boyd kupoteza fahamu kwa muda. Moyo wake ulikuwa kana kwamba umekatwa katwa na kisu chenye ncha kali. Boyd alishindwa kustahimili maumivu ya kumpoteza mke wake aliyebahatika kuzaa nae watoto wawili.

Michele Mumba alimuaga Boyd kuwa anaenda kumtembelea rafiki yake wa kike, Boyd aliamini hivyo. Kabla ya mauti hayajamfika Michele Mumba alionekana klabu moja na Reinford Kalaba. Zilikuwa habari za Usaliti zilizoacha nyufa kwenye moyo wa Boyd lakini habari hizi zilikuwa ni za neema kwa waandishi wa habari kwani ni habari iliyojitokeza kwenye kila gazeti Afrika.

Taharuki ilitanda kila kona ya Afrika. Dunia ilijiuliza maswali bila majibu lakini bahati njema Reinford kalaba ameshinda vita dhidi ya kifo. Ni wakati sasa wa kuiambia Afrika na dunia juu ya usaliti aliofanya.

Urafiki umegeuka kuwa chuki ndani ya moyo wa Boyd. Usaliti umeacha kovu lisiloweza kufutika.

Boyd hataki tena faraja anataka ukweli wote kutoka kwa Reinford kalaba. Reinford Kalaba ameshinda kifo lakini dunia inamsubiri kuthibitisha yote yaliyotawala kwenye vichwa vya magazeti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live