Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Refa wa Simba apewa dili FIFA

Jean Jacques Ndala Jean-Jacques Ndala.

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Refa mwenye kismati na mechi za kimataifa za Simba,  Jean-Jacques Ndala (36) kutoka DR Congo ameteuliwa kuchezesha mechi za mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia yatakayofanyika Saudi Arabia kuanzia Disemba 12 hadi 22 mwaka huu.

Katika orodha iliyotolewa jana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Ndala ni miongoni mwa marefa 24 ambao wameteuliwa kuchezesha mashindano hayo kutokea mabara tofauti huku Afrika ikitoa marefa wanne tu na yeye akiwa pekee wa kati.

Ukiondoa Ndala, Afrika imetoa marefa wawili wasaidizi wa pembeni ambao ni Noupue Elvis wa Cameroon na Maringule Arsenio wa Msumbiji huku mwingine akiwa ni  Adil Zourak kutoka Morocco ambaye atakuwepo upande wa usimamizi wa teknolojia ya usaidizi wa video kwa marefa (VAR).

Katika orodha ya marefa 24 ambayo imeteuliwa na FIFA kuchezesha mashindano hayo, marefa wa kati ni watano, 10 wasaidizi na nane wa VAR huku pia akiteuliwa refa mmoja kwa ajili ya kutoa sapoti kwa waamuzi hao.

Ndala amechezesha idadi ya mechi nne za Simba katika mashindano ya kimataifa ambapo katika hizo, mbili imeibuka na ushindi, moja imepoteza na imetoka sare katika mechi moja na inayokumbukwa na wengi ni ile ya mashindano ya African Football League dhidi ya Al Ahly ya Misri ambayo Simba ilitoka sare ya bao 1-1 ingawa ikaaga mashindano hayo kwa wapinzani wao kunufaika na kanuni ya faida ya bao la ugenini.

Mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia yatashirikisha klabu saba za mabara tofauti ambapo hadi sasa sita zimeshakata tiketi ya kushiriki ambazo ni Manchester City (England), Al Ahly (Misri), Urawa Reds (Japan), Club Leon (Mexico), Auckland City (New Zealand) na Al Ittihad (Saudi Arabia)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live